








Kacou Philippe alizaliwa Desemba 1972 huko Katadji, katika mji wa Sikensi ( Ivory Coast). Ni mtoto wa mkulima asiyejua kusoma na kuandika. Baada ya shule ya msingi, Kacou Philippe alimaliza tu miaka nne ya kwanza ya shule ya upili. Kuanzia 1992 hadi 2002, alitumia wakati wake mwingi kufanya kazi ya vibarua kwenye maeneo ya ujenzi.
Yote ilianza na maono aliyoona Aprili 24, 1993. Kwanza, aliwasiliana na kasisi wa Kikatoliki ili kuelewa maana ya maono hio. Kisha, alijiunga na Wabaptisti, ambao alikaa nao kwa muda wa miezi mitatu, kabla ya kukutana na harakati za William Branham, mwinjilisti wa Marekani. Ambapo alibaki na harakati hii kama mfuasi kawaida kutoka 1993 hadi 2002.
Kacou Philippe alianza mahubiri yake ya hadharani mnamo Julai 2002, kufuatia ono la pili la malaika aliloona mwaka wa 1993. Kacou Philippe anadai kuwa nabii-mjumbe wa kelele yausiku wa manane, kama ilivyoelezwa katika Mathayo 25:6.
Kulingana na Kacou Philippe, makanisa yote yanamtumikia shetani katika jina la Yesu Kristo. Anasimulia mara kwa mara maono mengine aliyoyaona mwaka 1993, ambapo anasema aliona viongozi wa kanisa wakiwa katika sura za ajabu: “Miili yao ilikuwa miili ya wanadamu, lakini vichwa vyao vilikuwa vichwa vya wanyama mbalimbali.” Hili lilizua mijadala na makabiliano ya kwanza.
Kacou Philippe alihubiri juu ya mafumbo kadhaa, kama vile: "Ikiwa Mungu aliharibu maovu yote katika gharika wakati wa Nuhu, ni jinsi gani uovu ulivuka gharika na kurudi Duniani baada ya gharika?" Mahubiri haya yalichapishwa kwa ukamilifu na gazeti la Kameruni. Kacou Philippe anatangaza kwamba maneno yake yana dhamani sawa na maneno ya manabii wa Biblia.
Kufuatana na Kacou Philippe, Kanisa linaanza na Yohana Mbatizaji, na huu ni ubatizo wa toba. Kisha unakuja ubatizo wa ondoleo la dhambi pamoja na mitume, kisha ubatizo wa kuhesabiwa haki kwa imani na Martin Luther, kisha ubatizo wa kuzaliwa upya kwa Kanisa baada ya mateso ya kwanza ya Warumi, kisha ubatizo wa kufanywa wana, kisha ubatizo wa kutakaswa na John Wesley, kisha ubatizo wa kuzaliwa upya na Upentekoste, kisha wa urejesho na William Branham na hatimaye ubatizo wa urejesho kwa hali ya kwanza naKacou Philippe. Na anadai kwamba mbali na hayo, ubatizo mwingine wowote ni wa uongo, hata kama unafanywa kwa jina la Yesu Kristo au kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu kwa kuzamishwa.
Kacou Philippe anaiona Biblia kama kioo cha kuangalia nyuma cha gari au kitabu cha historia. Kwake yeye, Biblia ni masalio ya historia ya kabla ya Ukristo na Kiyahudi na haiwezi kwa njia yoyote kutoa uzima wa milele. Anachoma matoleo yote ya Biblia anayoona kuwa hatari kwa imani, kama vile Tob, King James, Thompson, Scofield, na Louis Segond. Kacou Philippe anafafanua upya ni lipi Neno la Mungu, akitofautisha kati ya Neno la Mungu ambalo ni (kweli zilizofunuliwa) na theolojia ambayo ni (maarifa yanayopatikana kupitia akili).
Anafafanua upya uungu wa Yesu Kristo, kuungama dhambi ambayo inafaa kufanyika hadharani, nafasi ya wanawake katika Kanisa, ubatizo wa maji, Roho Mtakatifu, nabii, Biblia, uhusiano kati ya Kanisa na Serikali, na mambo mengine kadhaa ya Ukristo. Kwa sababu yahii, alikataa kwenda alipoitwa na Kurugenzi Kuu ya Ujasusi ya Ivory Coast. Anafafanua upya Ukristo wote katika kitabu kiitwacho Kitabu cha Nabii
Kacou Philippe, kilichochapishwa katika mabuku matatu na Éditions Édilivre nchini Ufaransa. Tazama gazeti: Le Jour Plus No. 3399 la Aprili 15, 2016 na gazeti la Le Sursaut Nambari la Aprili 15, 2016.
Mnamo Machi 2008, Kacou Philippe alileta pamoja jumuiya nzima ya kidini, pamoja na waandishi wa habari na wanachama wa mashirika ya kiraia, kwa ajili ya mkutano wa Ukristo. Ilikuwa ni hoja dhidi ya makanisa. Gazeti moja lilimwita mwalimu mkuu wa Neno la Mungu. Kufuatia mkutano huu, gazeti lingine lilikuwa na kichwa cha habari: "Nabii Awavua Nguo Wanaume wa Mungu." Kama William Branham, Kacou Philippe alizungumza juu ya uwepo wa nguvu isiyo ya kawaida, ambayo inayosababishwa na malaika wa Aprili 24, 1993.
Mnamo 2008, mahubiri ya Kacou Philippe yalianza kutafsiriwa katika lugha zingine. Magazeti yalichapisha mahubiri yake kwa ukamilifu, hata nje ya Côte d'Ivoire. Gazeti la Kamerun lilikuwa na kichwa cha habari: "Kacou Philippe, Nabii amekuja Kurekebisha Ukristo." Mijadala ilizuka katika vyombo vya habari kama vile Afrika No.1. Mijadala ilianza. Baadhi ya watu hujibu kwa njia za kujificha, ilhali wengine hujibu kwa uwazi na kwa jeuri. Bado wengine wanaenda mbali zaidi, wakichukua mafundisho ya Kacou Philippe moja baada ya jingine ili kuyapinga.
Mnamo Mei 13, 2016, Nabii Kacou Philippe alikamatwa nyumbani kwake na mamlaka ya Ivory Coast kwa kukaidi mamlaka ya serikali, kuchochea chuki za kidini, na itikadi kali za kidini. Alitumia siku nne mchana na usiku akiwa ameketi kwenye kiti katika makao makuu ya huduma ya kijasusi ya Ivory Coast. Kisha alikaa siku mbili mchana na usiku katika chumba cha chini cha makao makuu ya polisi ya Abidjan na miezi mitatu katika gereza kuu la Abidjan kabla ya kuachiliwa usiku wa Agosti 16, 2016, na kunyimwa haki zake za kiraia, ikiwa ni pamoja na marufuku ya miaka mitano ya kuhubiri Injili. Vyombo vya habari vya Togo na Cameroon vilielezea kesi hiyo kama isiyoeleweka. Baadaye, viongozi wa kidini wa Ivory Coast walikiri kuwa ni wao walipanga kukamatwa na kufungwa kwake.
Kulingana na Kacou Philippe, huduma yake ya kinabii ina awamu mbili kuu au utambulisho. Awamu ya kwanza, ambayo aliiona kuwa urithi kutoka kwa baba yake, William Marrion Branham, ni utimilifu wa Mathayo 25:6 na inahusisha mafunuo yote yaliyomo katika sura ya 1 hadi 154 ya kitabu chake, *Kitabu cha Nabii Kacou Philippe*. Na Awamu ya pili, ambayo inahusisha unabii, ndoto, na maono, inajumuisha mafunuo yaliyomo katika sura ya 155 hadi 162 ya kitabu chake. Sura ya 163, na idadi isiyojulikana ya sura kwa sasa, inahusisha shuhuda za uponyaji na miujiza zinazothibitisha huduma yake kupitia huduma mbalimbali za uponyaji katika nchi kadhaa duniani, ikifikia kilele cha utimilifu wa maono ya uwanja mkubwa aliokuwa nao mwaka wa 1993.
Kulingana na Kacou Philippe, ndoto na maono ni lugha takatifu kati ya miungu na wanadamu, ikiwa ni pamoja na Mungu Mwenye Mkuu. Analinganisha ndoto na maono na sheria za barabarani na alama za barabarani katika safari ya wanadamu kuelekea kwa Mungu; kwa hiyo, kupuuza ndoto au maono ni kupuuza Mungu anaye zungumuza nawe. Hivyo, kulingana na yeye, hili ni somo linalopaswa kushughulikiwa katika makanisa na dini zote duniani ili kudhihirisha umuhimu wa ndoto na maono kwa waamini. Hata hivyo, tafsiri ya ndoto na maono inapaswa kufanywa kwa hekima na tahadhari kubwa na kiongozi yeyote wa kidini, kwani ni zawadi kutoka kwa Mungu. Ingelifanyika hivyo.
Mnamo Juni 5, 2022, Kacou Philippe alipata maono ambapo malaika alimpa daftari la bluu na kumwagiza aende Afrika Kusini. Kwa wakati uliowekwa, alielewa kwamba daftari la bluu lilikuwa pasipoti na kwamba baada ya zaidi ya miaka 20 ya huduma bila kuondoka Ivory Coast, sasa Mungu alikuwa akimuamuru afanye safari za umishonari. Na kwamba alikuwa aende kwanza Afrika Kusini kuchukuwa karama ya uponyaji iliyoachwa na William Branham. Kupitia ndoto na maono kadhaa, alielewa kwamba alipaswa kuandaa huduma za uponyaji na miujiza bila malipo. Mnamo 2021, malaika alimwagiza asikubali kamwe pesa au zawadi kutoka kwa mtu yeyote, kwa sababu yoyote, wakati wa huduma zake za uponyaji.
Alianza huduma zake za kwanza za uponyaji nchini Afrika Kusini mnamo Machi 2025 katika miji kadhaa ikijumuisha Johannesburg, Pretoria, Middelburg na Zebediela, na Aprili 2025 nchini Zimbabwe baada ya kukumbana na matatizo madogo ya kupata viza. Huduma za uponyaji nchini Zimbabwe zilifanyika katika miji ya Harare na Bulawayo kuanzia Aprili 16 hadi 21, 2025.
Wagonjwa kadhaa, vipofu, waliopooza, vilema, wenye UKIMWI, na viziwi, walipona mara moja au siku kadhaa baadaye, kulingana na shuhuda nyingi. Magazeti kadhaa ya Afrika Kusini, Zimbabwe, Ivory Coast, Benin, Cameroon, na Afrika ya Kati, pamoja na machapisho makubwa kama vile Herald na Chronicle, yaliripoti kuhusu safari za Nabii Kacou Philippe kwenda Afrika Kusini na Zimbabwe. Kulingana na Kacou Philippe, safari yake ya kimishonari ya huko Afrika Kusini na badaaye ya Zimbabwe, na miujiza yake, ilikuwa sawa na ile ya William Branham mwaka 1951.
Kufanana huku kwa miujiza kunaweza kuthibitishwa kwa kusoma au kusikiliza sura ya 163 na 164 ya kitabu cha Nabii Kacou Philippe na kitabu cha ushuhuda rasmi, cha William Branham, Nabii anatembelea Afrika Kusini Julius Stadsklev. Kufanana huku kunaongoza kwenye hitimisho kwamba malaika wa Mto Ohio ndiye malaika yule yule aliye pamoja na Nabii Kacou Philippe.
Baada ya Zimbabwe, Kacou Philippe alikuwa ameandaa kutembelea Gabon mnamo Juni 2025 lakini serikali ya Gabon ilimunyima viza kwa sababu ya viongozi wa kidini ambao walionyesha chuki dhidi ya huduma za uponyaji bila malipo za Nabii Kacou Philippe kwa msingi wa sababu mbalimbali, lakini hasa sababu muhimu ya hali hii ya huduma hizi za uponyaji bila malipo ni utiifu kamilifu wa maagizo ya malaika katika ono la 2021. Hii ilisababisha kukataliwa kwa programu yake nchini Gabon na programu katika nchi zingine kama vile Benin, Togo, Cameroun, Congo Brazzaville, na Congo Kinshasa.
Imetafsiriwa kutoka https://plus.wikimonde.com/wiki/Kacou_Philippe
(Ilihubiriwa Jumapili asubuhi 2 Agosti 2003, huko Locodjro Abijan-Ivory Coast)
(Ilihubiriwa Jumapili 20 Oktoba 2002, huko Locodjro Abijan-Ivory Coast)
(Ilihubiriwa Jumapili 10 Novemba 2002, huko Locodjro Abijan-Ivory Coast)
(Ilihubiriwa Jumapili asubuhi Desemba 15 2002, huko Locodjro Abijan-Ivory Coast)
(Ilihubiriwa Jumapili asubuhi Desemba 2 2002, huko Locodjro Abijan-Ivory Coast )
(Ilihubiriwa Jumapili asubuhi mnamo novemba 02, 2003 pa Locodjro, Abidjan – Ivori-Coast)
(Ilihubiriwa Jumapili, mnamo januari, 12, 2003 pa Locodjro, Abidjan – Ivory-Coast)
(Ilihubiriwa Jumapili asubuhi mnamo mei 03, 2003 pa Locodjro, Abidjan – Ivory-Coast)
Iluhubiriwa Jumapili asubuhi Februari 23, 2005 huko Locodjro Abidjan-Ivory Coast
(Ilihubiriwa Jumapili asubuhi, tarehe 01 december 2002, pale Locodjro, Abidjan – Ivory-Coast)
(Ilihubiriwa jumapili asubuhi 27 Aprili, tena kwa 2006 huko Locodjro Abidjan-Ivory Cost)